Ezekiel 24:1-6

Chungu Cha Kupikia

1 aKatika mwaka wa tisa, mwezi wa kumi, siku ya kumi, neno la Bwana likanijia kusema: 2 b“Mwanadamu, weka kumbukumbu ya tarehe hii, tarehe hii hasa, kwa kuwa mfalme wa Babeli ameuzingira mji wa Yerusalemu kwa jeshi siku hii ya leo. 3 cIambie nyumba hii ya kuasi fumbo, na uwaambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Teleka sufuria jikoni; iteleke
na umimine maji ndani yake,

4 dWeka vipande vya nyama ndani yake,
vipande vyote vizuri,
vya paja na vya bega.
Ijaze hiyo sufuria kwa mifupa hii mizuri;

5 echagua yule aliye bora wa kundi la kondoo.
Panga kuni chini ya sufuria kwa ajili ya mifupa;
chochea mpaka ichemke
na uitokose hiyo mifupa ndani yake.

6 f“ ‘Kwa kuwa hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Ole wa mji umwagao damu,
ole wa sufuria ambayo sasa
ina ukoko ndani yake,
ambayo ukoko wake hautoki.
Kipakue kipande baada ya kipande,
bila kuvipigia kura.

Copyright information for SwhKC